Kamati Kuu ya Uratibu ya Mpango wa Pamoja wa Kigoma
Kigoma, 2 Oktoba 2025 –Kamati Kuu ya Uratibu wa Mpango wa Pamoja wa Kigoma (KJP) ilikutana wiki hii kupitia maendeleo yaliyopatikana na kuweka vipaumbele kwa mwaka ujao. Kikao hicho kiliendeshwa kwa pamoja na viongozi wa Serikali ya Mkoa wa Kigoma na Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, kikiwakutanisha wawakilishi kutoka serikali kuu na za mitaa, wadau wa maendeleo, pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyoshiriki.
Wawakilishi kutoka nchini Ireland na Norway walihudhuria kikao hicho pamoja na wenzao kutoka serikalini na Umoja wa Mataifa. Wanakamati walipitia kwa pamoja Taarifa ya Maendeleo ya mwaka 2024/25 sambamba na Tathmini ya Nusu Muhula, na wakapitisha mpango kazi wa pamoja kwa mwaka 2025/26. Majadiliano yalisisitiza mafanikio endelevu yaliyowezeshwa kupitia mchango wa pamoja kutoka Ireland na Norway kupitia Mfuko wa Kuongeza Kasi wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG Acceleration Fund).
Matokeo yaliyorekodiwa ni pamoja na: ongezeko la upatikanaji wa huduma za maji kikanda (kutoka 57% mwaka 2019 hadi 77% mwaka 2025), kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi wanaohudhuria shule ambapo upatikanaji wa chakula sasa umeongeza ushiriki hadi zaidi ya 90% katika shule zilizolengwa, kupungua kwa unyanyasaji wa kijinsia (kutoka 42.6% mwaka 2016 hadi 34.1% mwaka 2023), kuimarishwa kwa huduma za afya za jamii zinazochangia kupungua kwa visa vya malaria kali na rufaa, ongezeko la upatikanaji wa usajili wa watoto, na maendeleo katika uwezeshaji wa wanawake na vijana kiuchumi kupitia utambulisho rasmi, upatikanaji wa fedha na soko.
“Mpango wa Pamoja wa Kigoma unaonesha kile kinachowezekana pale uongozi wa serikali, wadau wa maendeleo na Umoja wa Mataifa wanaposhirikiana kwa karibu kuboresha maisha ya watu,” alisema Bi. Susan Ngongi Namondo, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa. “Kuzingatia mambo muhimu yaliyopatikana kutoka ripoti ya mwaka 2024/25 na Tathmini ya Nusu Muhula, mipango kazi ya mwaka 2025/26 inalenga kwenye vipaumbele vyenye athari chanya zenye ukubwa na endelevu ili jamii ziendelee kufaidika.”
Kwa kipindi kilichobaki cha mpango huo, washirika walithibitisha tena kipaumbele cha Afya na Lishe; Uondoaji wa Vurugu Dhidi ya Wanawake na Watoto; Kilimo na Uwezeshaji wa Kiuchumi; pamoja na Utawala Bora, huku wakiwa na msisitizo mkubwa juu ya umiliki wa serikali, ufadhili wa ndani, na ushirikishaji wa sekta binafsi ili kudumisha matokeo.
Mashirika ya UN yanayojihusisha katika Huu Mpango kazi