Taarifa kutoka kwa Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa – Kuhusu Uamuzi wa Marekani Kujiondoa katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa
08 Januari 2026
Taarifa kutoka kwa Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa – Kuhusu Uamuzi wa Marekani Kujiondoa katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameonesha masikitiko yake kufuatia tangazo lililotolewa na Ikulu ya Marekani kuhusu uamuzi wa nchi hiyo kujiondoa kwenye baadhi ya mashirika ya Umoja wa Mataifa.
Mara kwa mara, tumeisisitiza kuwa michango inayotolewa na nchi wanachama kwa bajeti kuu ya Umoja wa Mataifa na ile ya ulinzi wa amani, kama ilivyoidhinishwa na Baraza Kuu, ni wajibu wa kisheria kwa mujibu wa Katiba ya Umoja wa Mataifa. Hii ni pamoja na wajibu wa Marekani.
Mashirika yote ya Umoja wa Mataifa yataendelea kutekeleza majukumu yao kulingana na mamlaka waliyopewa na nchi wanachama.
Umoja wa Mataifa una jukumu la kuhakikisha tunawatumikia wale wanaotegemea huduma zetu. Tutaendelea kutekeleza majukumu yetu kwa moyo wa dhamira na uwajibikaji.
Stéphane Dujarric Msemaji wa Katibu Mkuu
Malengo yanayofanyiwa kazi kupitia mpango huu
Mashirika ya UN yanayojihusisha katika Huu Mpango kazi
RCO
Ofisi ya Mratibu Mkazi
Help us improve your experience.
We are upgrading this website platform to make it clearer,
faster and more accessible.
Can you take a two-minute survey to share your feedback and help shape this upgrade?