Mashirika ya Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania

FAO
Shirika la Kilimo na Chakula Duniani ndilo shirika maalum linaloongoza jitihada za kimataifa za kupambana na janga la njaa. Lengo letu ni kuwa na usalama wa chakula kwa watu wote na kuhakikisha kwamba watu wanapata chakula bora ili wawe timilifu na wenye afya bora.
IFAD
Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo umewekeza kwenye maendeleo ya watu vijijini kwa miaka 40 kwa kuwawezesha kupunguza umaskini, kuimarisha usalama wa chakula, kukuza lishe na kujenga moyo wa ustahimilivu miongoni mwa wananchi.
ILO
Shirika la Kazi Duniani (ILO) linasimamia kuimarishwa haki za kijamii na haki za kibinadamu na ajira zinazotambulika kimataifa kwa kuzingatia dhima ya kuanzishwa kwake kwamba haki za kijamii ni muhimu kwa amani ya kudumu kwa watu wote.
IOM
 Shirika la Kimataifa la Uhamiaji lilianzishwa mwaka 1951 na limejikita katika misingi inayozingatia utu na njia za kistaarabu katika masuala ya uhamiaji kwa kuhakikisha wahamiaji na jamii wananufaika. Shirika la IOM hushirikiana na wabia wengine katika jamii ya kimataifa.
UNEP
Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa ni mamlaka kiongozi kwenye masuala ya mazingira na ajenda ya ulimwengu ya mazingira, inakuza utekelezaji thabiti wa mwelekeo wa mazingira wa maendeleo endelevu ndani ya Mfumo wa Umoja wa Mataifa.
UN Women
UN Women ni chombo cha Umoja wa Mataifa kinachoshughulikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake. Bingwa wa ulimwengu wa wanawake na wasichana, UN Women ilianzishwa ili kuharakisha maendeleo katika kukidhi mahitaji yao ulimwenguni.
UNAIDS
 Hii ni Programu iliyobuniwa na Umoja wa Mataifa kupambana na VVU/UKIMWI, ambayo inaoongoza na kuhamasisha dunia kufikia malengo ya kiujumla ya kuzuia maambukizi ya VVU, tiba, huduma na matunzo kwa waathirika.
UNCDF
Mfuko wa Maendeleo na Mitaji wa Umoja wa Mataifa hufanya fedha za umma na za kibinafsi kutatua changamoto za masikini katika nchi 47 zilizo na maendeleo duni duniani (LDCs).
UNDP
Likiwa katika nchi zipatazo 170, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa linajishughulisha na vita dhidi ya umaskini huku likizingatia kuilinda sayari dunia. Husaidia nchi kukuza sera madhubuti, kuongeza ustadi,kuingia ubia na taasisi ili kuwe na maendeleo endelevu.
UNHCR
Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi, ni shirika la kimataifa lililojitolea kuokoa maisha, kulinda haki na kujenga maisha bora ya baadaye kwa wakimbizi, jamii zilizohamishwa kwa nguvu na watu wasio na utaifa.
UNIC
 Vituo vya Habari vya Umoja wa Mataifa vinawajibika kukuza uelewa wa umma katika kuunga mkono malengo na shughuli za Umoja wa Mataifa kwa kusambaza habari zinazohusu shughuli za Umoja huo kwa watu kila mahali, hasa katika nchi zinazoendelea.
UNIDO
UNIDO ni wakala maalum wa UN ambao unakuza maendeleo ya viwanda kwa kupunguza umaskini, utandawazi unaojumuisha na uendelevu wa mazingira.
WFP
Mpango wa Chakula Ulimwenguni ndio shirika linaloongoza la kibinadamu kuokoa maisha na kubadilisha maisha, kutoa msaada wa chakula katika dharura na kufanya kazi na jamii kuboresha lishe na kujenga uthabiti.
WHO
WHO inaongoza juhudi za kimataifa katika afya ya jamii inaratibu mwitikio wa ulimwengu kwa majanga ya kiafya, kutoa msaada wa kitaalam ili kupanua wigo wa afya kwa wote, kuwahudumia walio hatarini ili kila mtu, kila mahali apate nafasi sawa ya kuishi maisha yenye ustawi.