Katika siku ya wanawake duniani, tunasherehekea wanawake na wasichana duniani kote, na tunawapongeza kwa yote waliyofanikiwa katika kupigania usawa.
Wanawake na wasichan wamepata mafanikio makunwa – wameondoa vikwazo, wamevunja fikra potofu na kuchochea maendeleo kuelekea dunia yenye haki zaidi na usawa zaidi.
Lakini bado wanakabiliwa na vikwazo vikubwa. Mabilioni ya wanawake na wasichana wanakabiliwa na kuenguliwa, ukosefu wa haki na ubaguzi, ilhali janga lililojikita la ukatili dhidi ya wanawake lilikimomonyoa ubinamu.
Dunia yetu inaakisi milenia ya uhusiano wa kimamlaka uliotawaliwa na mfumo dume.
Na maendeleo yanashambuliwa, kwa haki za wanawake kurudishwa nyuma
Kwa kiwango cha sasa, usawa wa kisheria utapatikana miaka mia tatu ijayo.
Tunapaswa kusonga mbele haraka.
Katika siku ya wanawake duniani, tunashikamana na wanawake na wasichana wanaopigania haki, na kuazimia kuchagiza maendeleo.
Maudhui ya mwaka huu – wekeza kwa wanawake – yanatumbusha kuwa kutokomeza mfumo dume kunahitaji kuweko kwa fedha mezani.
Tunasaidia mashirika ya wanawake yaliyo mstari wa mbele.
Na tunapaswa kuwekeza kwenye miradi ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na kuchochea ujumuishaji wanawake na uongozi wa wanawake kwenye uchumi, teknolojia za kidijitali, ujenzi wa amani na hatua kwa tabianchi.
Yote hii inategemea kupatikana kwa fedha kwa ajili ya maendeleo endelevu ili nchi ziwe na fedha za kuwekeza kwa wanawake na wasichana.
Tunahitaji pia kuongeza idadi ya wanawake viongozi kwenye sekta ya biashara, Benki Kuu na Wizara za Fedha. Hii inaweza kusaidia kuchochea uwekezaji kwenye sera na miradi inayokidhi mahitaji ya wanawake na wasichana.
Haki za wanawake zimedhihirisha kuwa njia ya haki ya jamii zenye haki, amani na ustawi. Hii ni vema kwetu sote.
Kwa Pamoja, hebu na tuchukue hatua za haraka kufanya kuwa halisia.
Asante