Timu Yetu Tanzania

Stephen Bainous Kargbo Profile

Tipo Tito Nyabenyi

FAO
Representative
Mr. Kargbo is the UNIDO representative to Tanzania, Mauritius and the Secretariat of the East African Community (EAC). He has national and international work experience of over 30 years in teaching/research, organizational change and development work. He has held various positions in NGOs, academia and the UN system (UNDP and UNIDO). Before his current position, he worked in the UNIDO Regional Office in Ethiopia, overseeing operations in Burundi, Rwanda and Uganda, as well as activities related to the African Union Commission. Mr. Kargbo holds a B.Sc.in Agricultural Education from the University of Sierra Leone, M.Sc.in Rural Development and PhD in Agricultural Economics from the Georg-August University of Goettingen, Germany.
Mark Bryan Schreiner Photos

Mark Bryan Schreiner

UNFPA
Mwakilishi
Mark alijiunga na familia ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania akitokea Rwanda, ambako alikuwa na wadhifa kama Mwakilishi wa UNFPA kutoka 2017 hadi 2021. Kwa miongo miwili iliyopita, Mark amefanya kazi Umoja wa Mataifa kama kiongozi wa kipekee na mchechemuzi wa afya na maendeleo ya wanawake na vijana. Amefanya majukumu ya UNFPA katika Ofisi ya Kanda Ndogo ya Pasifiki katika Visiwa vya Fiji, Pakistani, Eritrea, Afrika Kusini, Nigeria na Divisheni ya Afrika katika Makao Makuu ya UNFPA huko New York. Mark pia amewahi kufanya kazi na Mpango wa Umoja wa Mataifa - Mazingira - UNEP nchini Kenya na pia katika Tume ya Uchumi na Jamii ya Umoja wa Mataifa huko Asia na Pasifiki nchini Thailand. Mark ameoa na ni raia wa Canada.
Shalini Bahuguna

Shalini Bahuguna

UNICEF
Mwakilishi
Shalini Bahuguna alishika wadhifa huu wa Mwakilishi wa UNICEF katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzisha (kuanzia) Desemba, 2019. Kabla ya kupokea jukumu hili, Bi. Bahuguna alikuwa Naibu Mwakilishi wa UNICEF huko Ethiopia, jukumu alilokuwa nalo tangu Agosti, 2016. Alijiunga na UNICEF kama Mkuu wa Sera ya Jamii huko Nigeria mwaka 2009 na pia alifanya kazi kama Naibu Mwakilishi wa UNICEF huko Myanmar. Bi. Bahuguna ni mtaalamu wa maendeleo mwenye uzoefu huko Asia na Afrika katika muktadha wa nchi mbalimbali. Alianza maisha yake ya kazi na AZISE ya Maji na Usafi wa Mazingira huko India na kisha kufanya kazi katika Serikali ya India—programu ya magezu ya sekta ya maji chini ya Benki ya Dunia. Ana uzoefu mkubwa kama msimamizi wa misaada na mtaalamu wa maendeleo ya jamii alioupata akifanya kazi na Indara ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID) katika nchi za India, China, Indonesia na Afghanistani.
Mkuu wa Ofisi ya Mratibu Mkazi

Shabnam Mallick

RCO
Mkuu wa Ofisi ya Mratibu Mkazi
Kabla ya kushika wadhifa huo nchini Tanzania, Bi. Mallick alikuwa Meneja wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Huduma za Miradi (UNOPS) huko Gambia. Vile vile alikuwa Mratibu wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Kudhibiti Janga la UVIKO-19 nchini Gambia. Bi. Mallick ana zaidi ya miaka 18 ya uzoefu wa kazi za maendeleo ya kimataifa, ambapo kati ya hiyo, miaka 12 ameitumia katika nchi zenye migogoro/zilizotoka katika migogoro, na kwa kiasi kikubwa ameshika nyadhifa za uongozi na program mbalimbali katika nchi za kipato cha chini na zile za kipato cha kati, madola yanayoendelea ya visiwa vidogo na nchi zilizo katika mpito. Alikuwa Naibu Mwakilishi Mkazi wa Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP)- (Programu na Uendeshaji) huko Guyana, Bhutan na Korea ya Kaskazini/DPRK.

Bi. Mallick amefanya kazi katika nchi (mbalimbali) zikiwemo Afghanistani, Darfur nchini Sudani (ambako alikuwa Kaimu Mkuu wa Ofisi), Visiwa vya Solomon (kama Ofisa Mkuu na Meneja wa Malengo ya Maendeleo Endelevu – MDG!) huko Pasifiki ya Kusini na Sri Lanka. Bi. Mallick pia amefanya kazi Washington DC katika Benki ya Dunia (Idara ya Kilimo na Maendeleo Vijijini), kwa ajili ya Idara ya USAID ya Ukuaji wa Uchumi na Biashara/Ofisi ya Wanawake katika Maendeleo; na Brookings Institution – Idara ya Sera ya Nje.