Kazi zetu kwenye muktadha wa Malengo ya Maendeleo Endelevu Tanzania

Jinsi UN inavyosaidia kwenye Malengo ya Maendeleo Endelevu Nchi Tanzania

Umoja wa Mataifa na washirika wake nchini Tanzania wanajitahidi kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu: Malengo 17 yaliyounganishwa na kabambe ambayo yanashughulikia changamoto kuu za maendeleo zinazowakabili watu nchini Tanzania na duniani kote. Mpango wa sasa wa Usaidizi wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDAP II) umejikita katika Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), kwa kuzingatia jamii zilizo hatarini zaidi. Kwa kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu, Umoja wa Mataifa na Serikali ya Tanzania, kwa pamoja wanatengeneza na kutekeleza programu, sera na njia bunifu za kufikia watu waliotengwa. Madhumuni ya pamoja ni kuhakikisha mgawanyo sawa wa mafanikio ya maendeleo katika makundi ya watu na katika mikoa yote, na kuchangia katika kufikia SDGs muhimu ambazo zitakuwa na matokeo chanya kwa watu wa Tanzania.

Mpango wa Maendeleo Endelevu Tanzania

Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ni wito wa kimataifa wa kuchukua hatua kukomesha umaskini, kulinda mazingira ya dunia na hali ya hewa, na kuhakikisha kwamba watu kila mahali wanaweza kufurahia amani na ustawi. Haya ndiyo malengo ambayo UN inafanyia kazi Tanzania: