Nelson Mandela alikuwa shujaa wa ujasiri na imani.
Kiongozi wa mafanikio makubwa na ubinadamu wa ajabu.
Mkuu wa nyakati zetu, ambaye urithi wake tunauheshimu zaidi kupitia vitendo:
Hatua ya kupuliza sumu ya ubaguzi wa rangi, ubaguzi na chuki;
Hatua za kuzima urithi wa ukikoloni;
Na hatua ya kukuza usawa, haki za binadamu na zaidi ya yote, haki ya kisheria
Leo, umaskini, njaa na ukosefu wa usawa vinaongezeka.
Nchi zinazama katika madeni.
Mgogoro wa mabadiriko ya Tabia nchi unaharibu maisha ya wale ambao wamefanya kidogo katika kuisababisha.
Na mfumo wetu wa kifedha wa kimataifa usiokuwa na usawa wa haki na uliopitwa na wakati hautekelezi matakwa yake kama ulivyo mfumo wa usalama duniani.
Nivitu ambavyo vipo katika uwezo wetu kutatua kila moja ya shida hizi.
Kwa hivyo, tunapoadhimisha maisha na urithi wa Nelson Mandela, tuchangamshwe na roho yake ya ubinadamu, utu na haki.
Tukasimame na wanawake na wasichana, vijana na watengeneza mabadiliko kila mahali. Na tuchukue hatua kujenga ulimwengu bora. Asante.
***