Taarifa kwa vyombo vya habari

Maafa Hanang Tanzania: UN iko bega kwa bega katika usaidizi, asema Milišić

11 Desemba 2023

Janga hilo limepoteza maisha ya watu, nyumba na miundombinu kuharibiwa, maelfu kutawanywa na kukosa makazi huku watu wengine hawajulikani waliko. Sasa serikali ya nchi hiyo imeomba msaada kwa umoja wa Mataifa ambao umesema uko tayari kusaidia Zlatan Milišić mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo akizungumza na Nafisa Didi afisa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania UNIC Dar es salaam amesema “Umoja wa Mataifa nchini Tanzania umeshitushwa sana na janga kubwa lililotokea kutokana na mafuriko na maporomoko ya udongo , ambapo hadi sasa imebainika kuwa takriban watu 65 wamepoteza m aisha, zaidi ya 100 wamejeruhiwa na pia cha kusikitisha zaidi ya kaya 1200 sawa na watu wapatao 5000 hadi 6000 wamepoteza nyumba zao.”

Kuhusu ombi la serikali ya Tanzania kupata msaada kutoka Umoja wa Mataifa bwana Milišić amesemaUmoja wa Mataifa umekuwa ukifanyakazi na serikali ofisi ya waziri mkuu kuwasaidia na kuimarisha udhibiti wa majanga na hatua za kuyakabili na tunatumai kuna maoni kutokana na juhudi zetu za pamoja katika hatua za haraka na za ufanisi kutoka kwa serikali katika dharura hii. Serikali ilichukua haraka hatua katika siku ya kwanza ya dharura hii, ilisaidia katika operesheni ya kutafita na kuokoa watu , imetoa msaada wa chakula na vifaa vingine kwa watu waliotawanywa.”

Mratibu huyo mkazi ameendelea kusema kwamba “Umoja wa Mataifa umekuwa katika mawasiliano na kuisaidia serikali tangu siku ya kwanza ya kuzuka zahma hii ya dharura, na pia ndani ya UN tumekuwa tukiratibu juhudi kuhusu hatua za kusaidia watu walioathirika na janga hili.” HABARI KAMILI BOFYA HAPA NA HAPA

Laurean

Laurean Kiiza

UNDGC
Afisa Kikosi Msaidizi

Mashirika ya UN yanayojihusisha katika Huu Mpango kazi

RCO
Ofisi ya Mratibu Mkazi
UNIC
Kituo Cha Habari cha Umoja wa Mataifa

Malengo yanayofanyiwa kazi kupitia mpango huu