Mukhtasari wa Programu ya Pamoja ya Kigoma ya Umoja wa Mataifa- Juni 2019
Programu ya Pamoja ya Kigoma (KJP) ni jitihada inayohusisha mashirika 16 ya Umoja wa Mataifa (UN) ambayo yamejikita kushughulikia sekta mbalimbali kwa lengo la kuchochea maendeleo katika Mkoa wa Kigoma. Mashirika hayo 16 yanafanya kazi kwa kushirikiana na sekretariati ya mkoa na serikali za wilaya kwa kuzingatia mahitaji ya kimaendeleo ya mkoa na uwezo wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania. Kwa ujumla, programu hii imejikita zaidi katika jamii za wenyeji na pia kwa wakimbizi na wahamiaji.
Mashirika 16 ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania yanayoshiriki yanashirikiana katika maeneo saba ambayo ni: nishati endelevu na mazingira; uwezeshaji vijana na wanawake kiuchumi; kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto; elimu kwa wasichana na wanawake vijana; usafi wa maji na mazingira (WASH); kilimo; na, Afya, VVU na UKIMWI na Lishe.