Ireland yatangaza mchango wa Euro milioni 3.85 kusaidia utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) nchini Tanzania
01 Agosti 2023
Ubalozi wa Ireland na Umoja wa Mataifa nchini Tanzania wanafurahi kutangaza mchango wa kwanza wa Ireland kwenda kwenye Mfuko mpya wa kuongeza kasi ya utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo enedelevu (SDGs) nchini Tanzania. Mchango huo uliotolewa ni Euro milioni 3.85 sawa na takriban bilioni 10.47 Tsh.
Mfuko wa kuongeza kasi ya utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo enedelevu (SDGs) Tanzania ni utaratibu wa ufadhili wa wadau wengi uliowekwa na Umoja wa Mataifa Tanzania na Serikali ya Tanzania kusaidia utekelezaji wa Mpango wa Ushirikiano wa Maendeleo Endelevu wa Umoja wa Mataifa (UNSDCF) kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 2022-2027. Mpango huu wa Ushirikiano umejikita katika kupunguza umaskini wa kimaeneo nchini Tanzania kupitia ukuaji wa kiuchumi na maendeleo endelevu na uchumi wa kijani.
Mchango wa Ireland kwenye Mfuko Mfuko wa kuongeza kasi ya utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo enedelevu (SDGs) Tanzania utasaidia mipango ya pamoja ya Umoja wa Mataifa na mipango inayoangazia maeneo mengi ya UNSDCF. Hii itajumuisha kuimarisha mikakati itakayosaidia wakulima wadogo, mikakati ya kuimarisha afya na lishe kwa ngazi ya jamii, pia kuboresha ushiriki wa wanawake katika kutunga sera. Ruzuku hii inakwenda sambamba na ahadi ya Ireland ya kusaidia Urekebishaji wa Mfumo wa Maendeleo wa UN katika ngazi ya nchi jambo ambalo linaendana na kanuni za Mkataba ya Ufadhili wa UN za mwaka 2019 zilizokubaliwa na Nchi Wanachama na Umoja wa Mataifa.
Ireland imekuwa ikiendesha shughuli zake Kigoma kwa miongo mitatu. Nimeona changamoto ambazo watu wake wanakabiliana nazo pamoja na uvumilivu wao mkubwa na ukarimu. Ireland inajitolea kuwa sehemu ya kujenga mustakabali wenye ujasiri na ustawi wa Kigoma. Kuendeleza usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake na wasichana ndio msingi wa kila kitu tunachofanya," alisema Balozi wa Ireland nchini Tanzania, H.E. Mary O'Neil. "Tunajua kutokana na uzoefu wetu wenyewe nchini Ireland kwamba kutenga wanawake kunasababisha mateso na kuzuia maendeleo. Kuwezesha uwezo wa wanawake ni muhimu kwa ukuaji wa kiuchumi na maendeleo endelevu. Ireland ni mfuasi thabiti wa mfumo wa mataifa mengi.
Nchini Tanzania, UN ina jukumu muhimu la kuunganisha watu na taasisi; maarifa na rasilimali. Tunatarajia kufanya kazi kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania na mfumo wa UN kutekeleza SDGs," aliongeza.
"Tunatoa shukrani zetu kwa Serikali na watu wa Ireland kwa mchango huu wenye thamani. Ireland imekuwa mshirika thabiti wa UN nchini Tanzania kwa miaka mingi, na tunafurahi sasa kuikaribisha Ireland kwenye Mfuko mpya wa kuongeza kasi ya utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo enedelevu (SDGs) Tanzania. Hatua hii inaonyesha ushirikiano imara kati ya Ireland na UN nchini Tanzania, na ahadi yetu ya pamoja ya kusaidia Tanzania kuendeleza utekelezaji wa SDGs na mtazamo wa kuhakikisha hakuna atakayeachwa nyuma," alisema Mratibu Mkazi wa UN nchini Tanzania, Bwana Zlatan Milisic
Tuna thamini sana msaada wa washirika wetu. Mchango wa Ireland unatuweka katika nafasi nzuri zaidi ya kutoa matokeo makubwa katika maeneo mbalimbali ya kazi zetu kwa njia iliyo na uratibu na mfuatano zaidi.